Thursday, March 2, 2017

AGUERO BADO YUPO NJIA PANDA CITY.

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Sergio Aguero amesema klabu hiyo bado haijazungumza naye kuhusu mustakabali wake. Tetesi za mustakabali wa nyota huyo wa kimataifa wa Argentina ziliibuka baada ya kupoteza nafasi yake kwa chipukizi mwenye umri wa miaka 19 Gabriel Jesus. Meneja wa City Pep Guardiola amesema anataka kumbakisha nyota huyo mwneye umri wa miaka 28 lakini Aguero ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2020, amesema hajafanya mazungumzo yeyote kuhusu yeye kubakia City. Aguero amefunga mabao manne katika mechi mbili baada ya kurejeshewa nafasi yake wakati Jesus alipopata majeruhi ya mguu ambayo yatamuweka nje mpaka msimu unamalizika. Aguero anahikilia nafasi ya tatu miongoni mwa wafungaji bora wa City akiwa na ambao 158, na kumfanya kuzidiwa na Eric Brook anayeshikilia nafasi ya kwanza kwa mabao 20. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alijiunga na City akitokea Atletico Madrid kwa kitita cha paundi milioni 38 mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment