MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imekata rufani kwa kamati ya saa 72 ya Shirikisho la Soka nchini-TFF kupinga kadi ya njano ya kwanza aliyopewa mshambuliaji wao Obrey Chirwa. Kadi hiyo aliyopewa Chirwa katika dakika ya 45 ilikuwa ni baada ya kufunga goli linaloleta utata mpaka muda huu ambapo mwamuzi Ahmada Simba alilikataa na kumlima kadi na baadae kidogo kufanya kosa la utovu wa nidhamu na kupatiwa kadi nyekundu. Uongozi wa Yanga umekataa rufaa hiyo kwenye kamati ya masaa 72 kuhusiana na kadi aliyopatiwa mshambuliaji wao wa kimataifa Chirwa aliyopatiwa katila dakika ya 45 baada ya mwamuzi kulikataa goli alilofunga. Baadhi ya viongozi wa Yanga waliokuwapo uwanjani walionesha kusikitishwa na tukio la kukataliwa kwa goli ma Chirwa kupewa kadi ya njano na kuamua kukataa rufaa haraka sana. Viongozi hao, walienda mpaka vyumba vya kubadilishia waamuzi na kumpatia kamisaa wa mchezo huo rufaa hiyo ili iweze kusikilizwa ndani ya masaa 72. Kwa sasa katika kikosi cha Yanga, Chirwa amekuwa tegemeo kubwa sana akiziba pengo la Mzimbabwe Donald Ngoma aliye majeruhi ya goti kwa takribani wiki tatu sasa. Mshambulaji wa Kimataifa kutoka Zambia Obrey Chirwa akitoka uwanjani baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting.
No comments:
Post a Comment