Friday, March 3, 2017

KADI MAALUMU ZA UTAMBULISHO KUTUMIKA KOMBE LA DUNIA URUSI.

MASHABIKI wa soka watalazimika kuingia na kadi za utambulisho katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na ile ya Shirikisho itakayofanyika majira ya kiangazi nchini Urusi, ikiwa ni hatua ya kupambana na uhuni katika soka. Katika michuano ya Euro 2016 kulikuwa na vurugu kati ya mashabiki wa soka wa Urusi na Uingereza jijini Marseille. Mwezi uliopita BBC ilitoa makala maalumu kubainisha mipango ya vurugu katika michuano ijayo ya Kombe la Dunia. Urusi inatarajia kutoa kadi maalumu ambazo zitatumika kwa ajili ya kuingilia viwanjani na zinaweza kutumika kama visa ya kuingilia nchini humo.

No comments:

Post a Comment