Friday, March 3, 2017

NGULI WA SOKA WA ZAMANI WA UFARANSA NA REAL MADRID AFARIKI DUNIA.

NGULI wa soka wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, Raymond Kopa amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85. Kopa ni mmoja wa nyota wa kikosi cha Real Madrid ambacho kilitawala soka la Ulaya katika michuano ya hamsini mwishoni. Katika kipindi hicho akiwa Santiago Bernabeu Kopa alishinda mataji matatu ya Kombe la Ulaya na pia kutwaa tuzo ya Ballon d’Or mwaka 1958. Kopa aliyekuwa kicheza nafasi ya ushambuliaji alianza soka lake huko kwao Angers ambapo ndipo alipokuwa akiishi mpaka mauti yalimpomkuta, kabla ya kuhamia Reims na baadae kwenda Madrid.

No comments:

Post a Comment