KARIBU mashabiki 100 wa Borussia Dortmund wamefungiwa kuingia viwanjani katika mechi za Bundesliga nchi nzima kwa muda wa miaka miwili baada ya polisi kuwakuta na vifaa vya kufanyia vurugu. Kundi la watu 88 walizuiwa wakiwa njiani kuelekea katika mchezo huko Darmstadt, Februari 11 na kurudishwa Dortmund, wiki moja baada ya mashabiki wa Dortmund kuwashambulia wanawake na watoto waliokwenda kushuhudia mechi dhidi ya RB Leipzig. Ofisa usalama wa Chama cha Soka Ujerumani-DFB, Hendrik Grosse Lefert amesema adhabu hiyo ilizingatia umri wa watu hao lakini pia mwa mujibu wa matukio yao huko nyuma. Kundi hilo lililofungiwa lilikutwa na miwako, kofia ngumu na glovu maalumu za michezo. Dortmund waliadhibiwa kufuatia tukio la Leipzig kwa kufungwa kwa jukwaa lake la upande wa kusini kwa mechi moja ambalo linaingiza mashabiki 24,000.
No comments:
Post a Comment