Friday, March 3, 2017

AFYA YA TORRES YAIMARIKA ARUHUSIWA HOSPITALI.

MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Fernando Torres afya yake imeimarika, ana fahamu na akili timamu baada ya kupata majeruhi ya kichwa katika sare ya bao 1-1 waliyopata dhidi ya Deportivo La Coruna. Nyota huyo wa zamani wa Liverpool na Chelsea alianguka vibaya katika dakika 85 kufuatia kusukumwa kwa nyuma na Alex Bergantinos wakati wakigombea mpira. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 32, alifanyiwa vipimo vingine mapema leo na kuthibitika hakupata madhara zaidi hivyo kuruhusiwa kutoka hospitalini. Akizungumza baada ya kutoka hospitali, Torres amesema lilikuwa tukio la kuogofya lakini ana matumaini atarejea tena uwanjani hivi karibuni. Katika mchezo huo Atletico walilazimika kumaliza wakiwa pungufu kufuatia kumaliza idadi ya wachezaji wote watatu wanaostahili kutumika kwa mchezo mmoja.

No comments:

Post a Comment