Tuesday, March 7, 2017

CONTE AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUTOLEWA SIFA.

MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte amewataka wachezaji wake kutulia baada ya kuifunga West Ham United kwa mabao 2-1 jana na kupiga hatua kubwa kuelekea katika ubingwa wa ligi Kuu. Chelsea wanaongoza kwa tofauti ya alama 10 dhidi ya Tottenham Hotspurs wanaoshika nafasi ya pili huku kukiwa kumebaki mechi 11 kabla ya msimu kumalizika. Mashabiki wa klabu hiyo jana walikuwa wakiimba nyimbo za ubingwa katika London, lakini Conte amesema wanapaswa kufikia jinsi ya kuchukua alama 26 zilizobakia kabla ya kujitangaza mabingwa. Akizungumza na wanahabari, Conte amesema wanapaswa kufikiri kila mpinzani watakayekutana naye anataka kuwafunga kuanzia sasa mpaka mwishoni. Conte aliendelea kudai kuwa mpaka sasa walipofika ni pazuri lakini jambo la muhimu ni kutojisahau na kuhakikisha wanaendeleza makali yao.

No comments:

Post a Comment