Tuesday, March 7, 2017

XAVI ATAMANI KUINOA BARCELONA.

NGULI wa soka wa zamani wa Barcelona, Xavi amedai ana ndoto za kuja kuinoa klabu hiyo lakini ameweka wazi kuwa hayuko katika mpango wa kuchukua nafasi ya Luis Enrique mwishoni mwa msimu huu. Enrique alibainisha wiki iliyopita kuwa taachia ngazi pindi msimu utakapokamilika baada ya kukaa Camp Nou kwa miaka mitatu huku baadhi ya watu wakimpigia chapuo Xavi kuwa mtu sahihi wa kuchukua nafasi hiyo. Hata hivyo, pamoja na kwamba nguli huyo mwneye umri wa miaka 37 anayecheza soka katika timu ya Al Sadd ya Qatar, anapenda kuja kuinoa Barcelona siku za usoni lakini ameondoa uwezekano wa kutua sasa hivi kwakuwa hana uzoefu wa kutosha bado. Xavi amesema bado kuna vingi vya kujifunza pale linapokuja suala la kuwaongoza wachezaji 25 na benchi zima la ufundi pamoja na madaktari.

No comments:

Post a Comment