Wednesday, March 15, 2017

MBIVU NA MBICHI KWA HAYATOU KUJULIKANA KESHO.

RAIS wa Shirikisho la Soka la AFrika-CAF, Issa Hayatou anatarajiwa kukabiliwa na upinzani mkubwa wakati akitafuta nafasi ya kuongoza kwa kipindi cha nane shirikisho hilo katika Mkutano Mkuu utakaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia kesho. Ahmad waziri wa serikali ya Madagascar ambaye anatumia jina moja ndio anatarajiwa kutoa upinzani kwa Hayatou katika uchaguzi akiwa ni mgombea wa tatu kushindana naye toka achaguliwe kuingoza CAF kwa mara ya kwanza mwaka 1988. Wagombea wengine waliowahi kugombea na Hayatou ni pamoja na Armando Machado wa Angola mwaka 2000 na Ismail Bhamjee wa Botswana mwaka 2004. Hata hivyo, Ahmad anakuwa mgombea wa kwanza kuungwa mkono na idadi kubwa ya wajumbe wa CAF likiwemo Baraza la Soka la nchi za Kusini mwa Afrika-COSAFA lenye wajumbe 14 pamoja na Nigeria.

No comments:

Post a Comment