Wednesday, March 15, 2017

GOTZE NJE MSIMU WOTE.

KLABU ya Borussia Dortmund imethibitisha kuwa maradhi ya Mario Gotze yatamuweka nje ya uwanja mpaka mapema msimu ujao. Mapema Februari ilitangazwa kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani, ambaye alifunga bao la ushindi katika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014, angekuwa nje ya uwanja kwa muda uziojulikana kutokana na maradhi yanayomsumbua. Lakini Dortmund ambao wiki iliyopita walifuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, sasa wamebainisha kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 hataweza kurejea tena msimu huu. Katika taarifa yake, Dortmund wamesema lengo lao kubwa ni kwa mchezaji huyo kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya msimu ujao.

No comments:

Post a Comment