MWENYEKITI wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge ameondoa uwezekano wa kumuuza Joshua Kimmich kwenda Manchester City. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 alikuwa akipata nafasi kwenye kikosi cha kwanza chini ya Pep Guardiola alipokuwa Allianz Arena msimu uliopita lakini hivi sasa amekuwa akipaa nafasi chache toka Carlo Ancelotti apewe mikoba. Kimmich alikuwa benchi katika mchezo wa Bundesliga walioshinda 3-0 dhidi ya Entracht Frankfurt mwishoni mwa wiki iliyopita na baadae kukiri suala la kukosa nafasi linaanza kumyima raha. Kufuatia hali tetesi zimekuwa zikiibuka kuwa Guardiola anaweza kumpeleka Etihad msimu ujao lakini Rummenigge amesisitiza kuwa wana mipango mikubwa na beki huyo hivyo hawataweza kumuuza kwasasa. Rummenigge amesema wana mipango mikubwa ya baadae kwa Kimmich kwani wanataka achukue nafasi ya Philipp Lahm anayetarajiwa kutundika daruga zake mwishoni mwa msimu huu.
No comments:
Post a Comment