Tuesday, March 14, 2017

JUVENTUS KUMCHUKUA SPALLETTI KAMA ALLEGRI AKIAMUA KUONDOKA.

KLABU ya Juventus bado inaendelea na jitihada kumshawishi Massimiliano Alegri kuendelea kubakia jijini Turin lakini wanaweza kumchukua Luciano Spalletti kama meneja huyo wa sasa akiamua kuondoka mwishoni mwa msimu. Mkataba wa Allegri unamalizika Juni 30 mwaka 2018 na Juventus wamekuwa wakifurahishwa na meneja huyo wa zamani wa AC Milan ambaye amefanikiw kushinda mataji mawili mfululizo ya Serie A toka achukue mikoba kiangazi 2014. Pande zote mbili zimeendelea kuwa na mahusiano mazuri ya kikazi na bodi ya Juventus bado ina matumaini ya kumbakisha meneja huyo katika klabu hiyo. Hata hivyo, Allegri bado ana wazo la kujaribu bahati yake nje ya Italia kutokana na kuwa tayari ameshinda mataji matatu la Serie A akiwa na Milan na Juventus. Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kuwa Arsenal inaweza kumuwania kufuatia meneja wake Arsene Wenger kuwa katika shinikizo kubwa hivi sasa.

No comments:

Post a Comment