Tuesday, March 14, 2017

TORRES KUREJEA UWANJANI KESHO.

MSHAMBULIAJI nyota wa Atletico Madrid, Fernando Torres anategemewa kurejea ikiwa zimepita wiki mbili pekee baada ya kuzimia kufuatia kugongwa kichwani, wakati kikosi chao kikijaribu kutafuta nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kesho. Atletico wanapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele kwa mwaka wan ne mfululizo kufuatia kushinda mabao 4-2 katika mchezo wao wa mkondo wa kwanza dhidi ya Bayer Leverkusen wiki tatu zilizopita. Torres amerejea mazoezini kwa mara ya kwanza Jumatatu toka alipozimia kufuatia kugongana na Alex Bergantinos wa Deportivo La Coruna. Akizungumza na wanahabari, Diego Simeone amesema wana imani Torres atakuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo.

No comments:

Post a Comment