Tuesday, March 14, 2017

ARSENAL KURUDIANA NA BAYERN NCHINI CHINA.

KLABU ya Arsenal imethibitisha kuwa watacheza mchezo wa kirafiki na Bayern Munich nchini China Julai mwaka huu. Arsenal watavaana na wababe wao hao waliowatoa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jijini Shanghai Julai 19 kabla ya kuja kukutana na Chelsea siku tatu baadae jijini Beijing katika Uwanja wa Bird’s Nest. Mpambano huo unaweza kuwa nafasi kwa Arsenal kulipa kisasi kufuatia kufungwa jumla ya mabao 10-2 na mabingwa hao wa Ujerumani katika mechi za mikondo miwili za michuano ya Ulaya. Ofisa mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis amesema mchezo huo utakuwa maalumu kwa ajili ya mashabiki wao wa China. Gazidis aliendelea kudai kuwa kumekuwa na mashabiki wengi nchini humo ndio maana wameamua kwenda kucheza mechi hizo mbili za kirafiki huko ili kuwazogezea burudani wanayoikosa.

No comments:

Post a Comment