Wednesday, April 19, 2017

ARSENAL YATHIBITISHA WILSHERE AMEVUNJIKA MGUU.

KLABU ya Arsenal imethibitisha kuwa Jack Wilshere ambaye yupo kwa mkopo Bournemouth, amevunjika mguu na anatarajiwa kukosa msimu wote uliosalia. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 aligongana na Harry Kane katika kipindi cha pili wakati Bournemouth walitandikwa mabao 4-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu na Tottenham Hotspurs Jumamosi iliyopita. Vipimo vimeonyesha kuwa Wilshere alivunjika mguu wake kama ilivyokuwa msimu uliopita na kusababisha kipindi kirefu kuwa nje ya uwanja. Katika taarifa yake, Arsenal walithibitisha taarifa hizo huku wakiongeza kuwa hataweza kurejea uwanjani mpaka msimu ujao.

No comments:

Post a Comment