Wednesday, April 19, 2017

MOURINHO AMUONYA MARTIAL.

MENEJA wa Manchester United, Jose Mourinho amemwambia Anthony Martial kuwa anatakiwa kufanya anachotaka kama anataka kufanikiwa kwenye klabu hiyo. Martial hakujumuishwa katika kikosi cha United kilichopambana na Chelsea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo kikosi cha Mourinho kiliibuka na ushindi mnono wa mabao 2-0 dhidi ya vinara hao wa Ligi Kuu ya Uingereza. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amefanikiwa kucheza kwa dakika 90 mechi tatu pekee za ligi msimu huu na Mourinho sasa amemuonya kuwa anatakiwa kufuata maelekezo yake kama anataka kufanikiwa. Akizungumza na wanahabari, Mourinho amesema wamekuwa pamoja kwa miezi 10 sasa hivyo anawafahamu wachezaji vizuri zaidi hivi sasa na wachezaji nao wanapaswa kumuelewa vyema sasa. Mourinho aliendelea kudai kuwa wachezaji wanapswa kufahamu ni kitu gani anataka na wao kufuata utaratibu huo. United inakabiliwa na mchezo dhidi ya Anderlecht kesho ukiwa ni mchezo wao wa mkondo wa pili wa robo fainali ya Europa League baada ya kutoka sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza huko Ubelgiji.

No comments:

Post a Comment