Wednesday, April 19, 2017

TERRY AGOMA KUSTAAFU PAMOJA NA KUONDOKA CHELSEA.

BEKI wa Chelsea, John Terry amesisitiza hana mpango wa kustaafu wakati atakapokamilisha uamuzi wake mgumu kuwahi kufanya maishani kwa kuondoka kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu. Terry alibainisha mapema wiki hii kuwa ataondoka rasmi Chelsea baada ya kupita miaka 19 akiitumikia pindi msimu utakapomalizika. Uamuzi wa beki huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 36 uliibua hisia kuwa anaweza kuamua kutundika daruga zake baada ya kucheza mechi tano pekee kwa Chelsea msimu huu. Hata hivyo, Terry alifafanua katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa uamuzi wa kuondoka Chelsea ulikuwa kufanya kwenye maisha yake lakini anadhani ulikuwa wakati sahihi kufanya hivyo. Kikubwa kilichomfanya kuondoka Chelsea ni uhakika wa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwani bado anadhani anataka kuendelea kucheza soka. Terry ameshinda mataji 14 akiwa na Chelsea huku akicheza mechi 713 toka alipojiunga kwa mara ya kwanza mara 1998.

No comments:

Post a Comment