Wednesday, April 19, 2017

RONALDO AWATAKA MASHABIKI WA MADRID KUMPA HESHIMA YAKE.

MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amewataka mashabiki kumpa heshima zaidi baada ya kufunga hat-trick katika ushindi wa mabao 4-2 waliopata kwenye mchezo wao wa marudiano dhidi ya Bayern Munich jana. Katika wiki za karibuni Ronaldo alikuwa hafungi mabao kama ilivyozoeleka na kupeleka baadhi ya mashabiki kumzomea kwa kudhani kuwa hajitumi ipasavyo. Lakini jana mashabiki wote walikuwa wakishangilia jina lake mwishoni baada ya kuisaidia Madrid kupata ushindi huo ambao umewapeleka katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa jumla ya mabao 6-3. Akizungumza na wanahabari Ronaldo amesema hajawazi kuwaambia mashabiki wanyamaze, alichotaka kuwaambia yeye ni kuacha kuzomea kwasababu siku zote amekuwa akijituma kwa bidii ili kuisaidia timu.

No comments:

Post a Comment