Wednesday, April 19, 2017

NEUER KUKOSA MSIMU ULIOSALIA.

KIPA wa Bayern Munich, Manuel Neuer anatarajiwa kukosa msimu wote uliosailia baada ya kuumia mguu wake wa kushoto katika kipigo cha mabao 4-2 walichopata kutoka kwa Real Madrid jana. Nahodha huyo wa kimataifa wa Ujerumani alipata majeruhi hayo wakati akijaribu bila mafanikio kumzuia Ronaldo kufunga bao la tatu kwenye dakika ya 109 katika Uwanja wa Santiago Bernabeu. Ofisa mkuu wa Bayern , Karl-Heinz Rummenigge alithibitisha taarifa hizo mara baada ya mchezo huo uliokwamisha ndoto zao za kwenda nusu fainali. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki nane hivyo kuzusha hofu pia ya kuweza kuikosa michuano ya Kombe la Shirikisho inayotarajiwa kuanza Juni 17.

No comments:

Post a Comment