Monday, April 17, 2017

CHIELLINI AWAONYA WACHEZAJI WENZAKE KUHUSU MSN.

BEKI wa Juventus, Giorgio Chiellini ameonya kuwa nyota wa Barcelona Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar ni kama papa ambao wanaweza kuwamaliza. Vigogo hao wa Turin wanaongoza kwa mabao 3-0 ushindi waliopata kwenye mchezo wao wa mkondo wa kwanza wa robo fainali wakati Paulo Dybala alipong’aa kwenye mchezo huo huku safu ya ushambuliaji wa Barcelona inayojuliakana kama MSN ikishindwa kutamba kabisa. Messi, Suarez na Neymar wote walifunga wakati Barcelona walipoweka historia katika hatua ya 16 bora baada ya kutoka nyuma wakiwa wamefungwa mabao 4-0 na Paris Saint-Germain na kuja kushinda mchezo wa marudiano Camp Nou kwa mabao 6-1. Chielini amewaonyesha wachezaji wenzake kufanya kila wawezalo kuhakikisha suala hilo halijirudii kwenye mchezo wao wa Jumatano. Akizungumza na wanahabari, Chiellini amesema kama wakifanikiwa kuwaweka nyota wa Barcelona mbali na eneo lao la hatari ni wazi wanaweza kuondoka na chochote kwenye mchezo huo. Chiellini aliendelea kudai kuwa Barcelona ina safu bora ya ushambuliaji duniani na kama wakinusa wakiona kuna uwoga fulani haraka wanaweza kukuadhibu kama papa anavyonusa harufu ya damu.

No comments:

Post a Comment