Monday, April 17, 2017

BALE KUIKOSA BAYERN.

MENEJA wa Real Madrid, Zinedine Zidane amethibitisha kuwa watamkosa winga wao Gareth Bale kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kesho dhidi ya Bayern Munich. Bale alitolewa katika kipindi cha pili wiki iliyopita kwenye ushindi wa mabao 2-1 waliopata dhidi ya mabingwa hao wa Bundesliga kule Allianz Arena huku pia akikaa nje kwenye mchezo dhidi ya Sporting Gijon walioshinda mabao 3-2 Jumamosi iliyopita. Nyota huyo wa kimataifa wa Wales ameshakaa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi mitatu kutokana na majeruhi ya kifundo cha mguu. Akizungumza na wanahabari, Zidane amesema Bale amefanya jitihada kubwa za kurejea na kucheza baada ya kukaa nje kwa muda lakini amepata matatizo kidogo ndio maana ameamua kumpumzisha. Zidane aliendelea kudai kuwa ana matumaini ndani ya siku chache atakuwa fiti lakini kesho hatakuwa tayari.

No comments:

Post a Comment