Wednesday, April 5, 2017

AS ROMA YAMUWANIA MANCINI.

KLABU ya AS Roma imeripotiwa kufanya mawasiliano na Roberto Mancini kuhusu kuchukua nafasi ya Luciano Spalletti, huku akikubali kupunguza kiwango cha mshahara anachohitaji. Kwasasa kocha huyo anatarajiwa kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu na amekataa kujadili mustabali wake wa baadae. Hatua hiyo imezusha tetesi kuwa Spalletti ataondoka mwishoni mwa msimu huu huku klabu hiyo ikidaiwa kuhaha kutafuta mbadala wake. Taarifa kutoka nchini Italia zinadai kuwa Roma wamezungumza na Mancini ambaye yuko tayari kushusha kiwango cha mshahara wake chini ya euro milioni 4.5 alizokuwa akichukua alipokuwa Inter Milan.

No comments:

Post a Comment