Wednesday, April 5, 2017

WATATU WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA UPANGAJI MATOKEO.

POLISI nchini Hispania imekamata watu wengine watatu wakiwemo wachezaji wawili kuhusiana na uchunguzi wa upangaji wa matokeo wa klabu ya CD Eldense. Wachunguzi tayari wanamshikilia kocha wa klabu hiyo ya daraja la tatu Filippo Vito di Pierro na Mkurugenzi Mkuu Nobile Capuani. Kukamatwa huko kumekuja kufuatia Eldense kuchapw amabao 12-0 mwishoni mwa wiki iliyopita na Barcelona B huku klabu hiyo ikichapwa mabao matano baada ya dakika 15 huku mpaka mapumziko wakitandikwa mabao 8-0. Shirikisho la Soka la Hispania-RFEF ilitangaza kufungua kesi dhidi ya Eldense kwa suala la upangwaji matokeo.

No comments:

Post a Comment