Wednesday, April 5, 2017

CHAPECOENSE WAICHAPA ATLETICO NACIONAL.

KLABU ya Chapecoense imefanikiwa kuifunga Atletico Nacional kwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa Supercup ya Amerika Kusini uliofanyika jana. Mchezo huo ulitoa kumbukumbu ya wachezaji waliokufa katika ajali ya ndege kabla ya timu hiyo haijacheza mchezo wa fainali ya Copa Sudamericana Novemba mwaka jana. Mchezo huo ni wa kwanza kati ya timu hizo toka wachezaji wote kasoro watatu kwenye timu hiyo ya Brazil na viongozi wao kufariki kwenye ajali ya ndege wakati wakikaribia Medellin mwaka jana. Watu sita pekee kati ya 77 waliokuwepo kwenye ndege ndio waliopona kwenye ajali hiyo. Kabla ya mchezo huo wa jana timu zote pamoja na mashabiki walisimama kwa dakika moja kuwakumbuka wote waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo. Mchezo wa marudiano baina ya timu hizo unatarajiwa kufanyika Mei 10 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment