Wednesday, April 5, 2017

SIJALI WANAONIKOSOA - MESSI.

MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amesisitiza kuwa hafuatilii wale wote wanaokosoa kiwango chake akiwa na timu ya taifa ya Argentina. Messi amekuwa na msimu mzuri Camp Nou lakini ameshindwa kupeleka mafanikio hayo kwenye timu ya taifa. Nyota huyo alitwaa medali ya dhahabu mwaka 2008 lakini walijikuta wakishindwa kwenye fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014 pamoja na fainali mbili za Copa America mwaka 2015 na 2016. Akizungumza na wanahabari, Messi amesema huwa hajali sana wanaomkosoa kwani anafahamu kitu gani kinaendelea. Messi aliendelea kudai kuwa anafahamu kuwa watu siku zote wanataka washinde na kuleta mataji nyumbani.

No comments:

Post a Comment