Tuesday, April 4, 2017

NILISHANGAA NILIPOPEWA JEZI NAMBA 7 NA FERGUSON - RONALDO.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema alishangazwa wakati Sir Alex Ferguson alipomwambia avae jezi namba saba akiwa Manchester United, akifuata nyayo za manguli kama kina George Best, Eric Cantona na David Beckham. Akizungumza na wanahabari, Ronaldo amesema wakati ametua United alikuwa amepanga kuvaa jezi namba 28 lakini Ferguson alimwambia angependa avae namba saba. Ronaldo aliendelea kudai kuwa jambo hilo lilimshangaza kwasababu alikuwa anafahamu wachezaji wakubwa waliowahi kuvaa jezi yenye namba hiyo. Ronaldo ambaye alikuwa na umri wa miaka 18 pekee wakati akitua Old Trafford akitokea Sporting Lisbon mwaka 2003, alikwenda kushinda mataji matatu ya Ligi Kuu na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Pia Ronaldo alipata tuzo yake ya kwanza ya Ballon d’Or akiwa United kabla ya kuhamia Madrid mwaka 2009 kwa kitita cha euro milioni 94.

No comments:

Post a Comment