Tuesday, April 4, 2017

WENGER ADAI KUMAIZA NAFASI NNE ZA JUU SIO RAHISI KAMA INAVYOFIKIRIWA.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kusuasua kwa kikosi chake msimu huu kunaonyesha kwamba kumaliza kwenye nafasi nne za juu katika Ligi Kuu sio jambo rahisi kama inavyofikiriwa. Meneja huyo raia wa Ufaransa ameiongoza Arsenal kumaliza kwenye nafasi nne na kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita. Lakini huku kukiwa kumebaki mechi 10, Arsenal kwasasa wanashikilia nafasi ya sita, alama saba nyuma ya kufikia nafasi ya nne. Akizungumza na wanahabari, Wenger amesema kumaliza kwenye nafasi nne itakuwa changamoto nzuri lakini anafikiri ni jambo linalowezekana. Wenger aliendelea kudai kuwa wamekuw wakifanya hivyo kwa miaka 20 na ilionekana kama sio kitu lakini amefurahi kuona watu wakigundua kuwa sio rahisi kama inavyofikiriwa.

No comments:

Post a Comment