Tuesday, April 4, 2017

ODEMWINGIE ATIMKIA INDONESIA.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Nigeria, Peter Odemwingie angependa kurejesha makali nchini Indonesia kwa kufunga mabao muhimu baada ya kusajiliwa na klabu ya Madura United. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 35 ambaye aliiwakilisha Nigeria katika michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2010 na 2014, amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo huku kukiwa na kipengele cha kuongezewa mwingine. Odemwingie amekuwa bila klabu toka alipoondoka Rothertham Januari mwaka huu. Akizungumza na BBC Odemwingie anafurahi kuwa sehemu ya kipindi kizuri cha mapinduzi ya soka la Indonesia. Odemwingie aliendelea kudai kuwa ana matumaini makubwa ya kurejesha kiwango chake kwa kuifungia Madura mabao muhimu. Odemwingie amekuwa mchezaji wa tatu aliyewahi kuichezea Ligi Kuu ya Uingereza kwenda Indonesia baada ya Michael Essien na Carlton Cole.

No comments:

Post a Comment