Tuesday, April 4, 2017

IBRAHIMOVIC AMALIZA ADHABU YA KUTOCHEZA MECHI NNE.

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amefurahi kurejea kwenye kikosi cha timu hio baada ya kumaliza adhabu yake kufungiwa mechi tatu za Ligi Kuu ya Uingereza. Nyota huyo wa kimataifa wa Sweden alilazimika kuwa mtazamaji kwa wiki kadhaa baada ya kulimwa adhabu hiyo na Chama cha Soka cha Uingereza-FA kwa kumpiga kiwiko beki wa Bournemouth Tyrone Mings katika sare ya bao 1-1 Machi 4 mwaka huu. Kutokuwepo kwake kumeshuhudia United wakitolewa kwenye michuano ya Kombe la FA dhidi ya Chelsea na kupoteza alama mbili kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya West Bromwich Albion mwishoni mwa wiki iliyopita. Akizungumza na wanahabari, Ibrahimovic amesema kukosekana kwake uwanjani ni sehemu ya mchezo kwani siku zote mchezaji hawezi kucheza kwasababu kuna muda unaweza kuumia au kutumikia adhabu kama yeye. Ibrahimovic aliendelea kudai kuwa anajisikia vyema na ana hamu kubwa ya kurejea uwanjani huku akiwa na matumaini ya kuendelea kuisaidia timu yake kwa kufunga mabao.

No comments:

Post a Comment