MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema hafahamu jinsi gani suala la kujitoa kwa Uingereza kwenye Umoja wa Ulaya likavyokuwa lakini ameongeza kama hawatahitaji wageni wataondoka. Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa may ameanza kuchukua hatua za kujitoa kwneye umoja huo mapema wiki hii na sasa watakuwa na miaka miwili ya kujadili jinsi ya kuondoka kwao. Moja ya mambo yatakayojadiliwa mpaka ifikapo mwaka 2019 ni pamoja na haki za raia wa EU wanaoishi Uingereza pamoja na raia wa Uingereza wanaoishi EU. Akiulizwa kuhusiana na suala hilo, Guardiola amesema anadhani hata Waingereza wenyewe wanasubiria kuona jinsi itakavyokuwa baada ya kujitoa. Guardiola aliendelea kudai kuwa jambo muhimu ni kusubiri ba kuona itakavyokuwa na kama wageni watalazimika kuondoka badi watafanya hivyo.
No comments:
Post a Comment