Saturday, April 1, 2017

WEST HAM WAMNYATIA LUCAS PEREZ.

KLABU ya West Ham United inadaiwa kumuwania mshambuliaji wa Arsenal Lucas Perez ambaye anadaiwa kutokuwa na furaha kwenye klabu hiyo. West Ham tayari wamshaweka mipango ya kumuwania Perez ambaye amepanga kuondoka Emirates majira ya kiangazi baada ya kushindwa kung’aa katika msimu wake wa kwanza Arsenal. Perez mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na Arsenal Agosti mwaka jana kwa kitita cha paundi milioni 17 kutoka Deportivo La Coruna lakini ameshindwa kupata namba ya kudumu kwneye kikosi hicho hivyo anataka kuondoka. West Ham wana matumaini kumpata mshambuliaji huyo kwa kiasi kama alichonunuliwa na Arsenal na inadaiwa tayri wawakilishi wa pande zote mbili wameshaanza mazungumzo.

No comments:

Post a Comment