Saturday, April 1, 2017

MATA KUKAA NJE WIKI KADHAA.

KIUNGO wa Manchester United, Juan Mata anatarajiwa kukaa nje kwa wiki kadhaa baada ya kufanyiwa upasuaji wa mtoki Alhamisi iliyopita. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania anatarajiwa kukosa mechi tatu za Ligi Kuu za United wiki hii na kuna hatihati ya kukosa mchezo wa mkondo wa kwanza wa michuano ya Europa League dhidi ya Anderlecht. Kuanzia wiki ijayo atafanyiwa vipimo zaidi, ingawa Mata mwenyewe ana uhakika wa kurejea uwanjani kabla ya kumalizika kwa msimu huu. Majeruhi yameathiri safu ya kiungo ya United kufuatia Paul Pogba na kuwa majeruhi wakati Ander Herrera na mashabuliaji Zlatan Ibrahimovic wakitumikia adhabu.

No comments:

Post a Comment