Tuesday, April 25, 2017

BALE KUIKOSA ATLETICO MADRID.

KLABU ya Real Madrid imethibitisha kuwa winga wao Gareth Bale atakosa mechi za nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid kutokana na majeruhi yanayomsumbua. Klabu hiyo imedai kuwa nyota huyo anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kisichopungua wiki tatu hivyo wanamtegemea kurejea uwanjani katikati ya mwezi Mei. Taarifa hiyo inamaanisha kuwa Bale mwenye umri wa miaka 27 atakosa mechi za mikondo yote miwili za Madrid hidi ya majirani zao Atletico. Katika taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa kupitia tovuti yake imedai kuwa kufuatia vipimo alivyofanyiwa Bale amegundulika kuwa alipata majeruhi ya msuli wa kigimbi na maendeleo yake yatakuwa yakifuatiliwa kadri siku zinavyokwenda. Mbali na mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya, Bale pia atakosa mechi za La Liga ambazo Madrid watacheza Valencia, Granada, Sevilla na Malaga.

No comments:

Post a Comment