Friday, April 7, 2017

COLE AFANYIWA UPASUAJI KUPANDIKIZA FIGO.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United, Andrew Cole amefanyiwa upasuaji kupandikiza figo. Nguli huyo mwenye umri wa miaka 45, ambaye aliwahi kuzichezea Newcastle United na Blackburn Rovers alipata matatizo ya figo baada ya kupata vurusi vya airborne mwaka 2015. Msemaji wa klabu ya United amesema upasuaji huo ni sehemu ya matibabu ya maradhi hayo yanayomsumbua nguli huyo. Msemaji huyo aliendelea kudai kuwa Cole kwasasa atachukua likizo ya muda katika kibarua chake kama balozi wa klabu hiyo. Akiwa Old Trafford, Cole alifunga mabao 121 katika mechi 275, nab ado anaendelea kuwa mchezo wa tatu mwenye mabao mengine zaidi kwenye Ligi Kuu akiwa mabao 187.

No comments:

Post a Comment