Friday, April 7, 2017

SANCHEZ KUIPA ARSENAL NAFASI NYINGINE.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema Alexis sanchez anataka kuendelea kubakia kwenye klabu hiyo kama wakiweza kufikia makubaliano. Nyota huyo wa kimataifa wa Chile mwenye umri wa miaka 28 ana mkataba wa unaomalizika majira ya kiangazi mwaka 2018, huku baadhi ya magazeti yakidai anataka kujiunga na Chelsea. Akizungumza na wanahabari, Wenger amesema anaamini kuwa Sanchez anataka kubaki hivyo itakuwa ni juu ya wakla wake kufikia makubaliano na klabu. Sanchez alijiunga na Arsenal akitokea Barcelona kwa kitita cha paundi milioni 35 kiangazi mwaka 2014 na amefunga mabao 22 msimu huu akiwa na timu hiyo. Wakati huohuo, Wenger amesema klabu ndio itakayotangaza mustakabali wake lakini mpaka sasa hajajua itakuwa lini. Meneja huyo amekuwa katika shinikizo kubwa hivi karibuni huku baadhi ya mashabiki wakimtaka ajiuzulu nafasi yake hiyo kutokana na timu hiyo kusuausua.

No comments:

Post a Comment