Friday, April 7, 2017

KLOPP ATAMANI KIKOSI CHA CHELSEA.

MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp anataka kikosi chake kuwa kama vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza Chelsea. Chelsea walipiga hatua kubwa kuelekea ubingwa kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manchester City Juzi, wakiendelea kuongoza kwa tofauti ya alama saba juu ya Tottenham Hotspurs waliopo kileleni. Kwa upande wa Liverpool wao hali ilikuwa tofauti kwani walijikuta waking’ang’aniwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Bournemouth na kuwafanya kubaki nafasi ya tatu huku wakiwa nyuma ya Chelsea kwa tofauti ya alama 12. Akiulizwa kama lolote la kujifunza kutoka kwa vinara hao wa ligi, Klopp amesema ni kweli wana cha kujifunza kwani hawana uzoefu wa kutosha kulinganisha na timu zingine. Liverpool wamebaikisha mechi saba, moja zaidi ya City waliopo chini yao wakati nafasi ya tano wapo Arsenal na Manchester United nafasi ya sita huku wakiwa na mechi mbili mkononi.

No comments:

Post a Comment