Friday, April 7, 2017

KANTE AMPIGIA CHAPUO HAZARD KUTWAA TUZO YA PFA.

KIUNGO wa Chelsea, N’Golo Kante amempigia chapuo mchezaji mwenzake Eden Hazard kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka ya PFA. Kante mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akipigiwa chapuo kushinda tuzo hiyo kwa msimu huu kutokana na kiwango bora alichoonyesha akiwa na vinara hao wa Ligi Kuu. Lakini kiungo huyo wa zamani wa Leicester City anaamini Hazard, ambaye alitwaa tuzo hiyo ya PFA kwa msimu wa 2014-2015, anastahili tena tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 13 na kuweka rekodi ya assists tano. Akizungumza na wanahabari kuhusiana na suala hilo, Kante amesema kwa upande wake ni rahisi kwani kila mtu ameona mambo makubwa anayofanya Hazard.

No comments:

Post a Comment