Friday, April 7, 2017

ISCO AKANUSHA TETESI ZA BARCELONA.

KIUNGO wa Real Madrid, Isco amekanusha kuwa na nia ya kujiunga na Barcelona na kuwalaumu marafiki zake kwa utata uliotokea kuhusiana na suala hilo. Isco mwenye umri wa miaka 24 alituma picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na marafiki zake wakila chakula cha mchana huku kukiwa na paketi ya vitafunwa yenye nembo ya Barcelona pembeni ya meza yao.  Muda mfupi baadae picha hiyo ilitengenezwa na kuwekwa nyingine inayofanana na hiyo ila ikiwa haina vitafunwa jambo ambalo lilizua mjadala wa mustakabali wa kiungo huyo. Hata hivyo, Isco aliondoa ukakasi huo na kudai kuwa hana mpango wowote kwa kwenda Barcelona.

No comments:

Post a Comment