Friday, April 7, 2017

MANE KUKOSA MECHI ZOTE ZA LIVERPOOL ZILIZOSALIA MSIMU HUU.

MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Sadio Mane anatarajiwa kukosa mechi zote saba zilizosalia msimu huu kwa klabu hiyo kutokana na majeruhi ya goti. Mane mwenye umri wa miaka 24, alitolewa nje ya uwanja baada ya kugongana na Leighton Baines Jumamosi iliyopita wakati waliposhinda mabao 3-1 nyumbani dhidi ya Everton. Meneja wa klabu hiyo Jurgen Klopp amesema ana uhakika kuwa Mane atahitaji kufanyiwa upasuaji hivyo kuondoa uwezekano wa kucheza tena msimu huu. Nyota huyo aliyesajiliwa kwa paundi milioni 34 kutoka Southampton ameanza katika mechi zote kasoro tano za Liverpool msimu huu. Klopp pia amesema Adam Lallana anaendelea vyema lakini hajaanza mazoezi na nahodha Jordan Hunderson naye yuko njiani kurejea uwanjani.

No comments:

Post a Comment