MAELFU ya wananchi wa Afrika Kusini wameingia mitaani leo nchi nzima wakipinga mabadiliko yaliyofanywa na Rais Jacob Zuma katika Baraza la Mawaziri. Mabadiliko ya naafsi muhimu za kisiasa, ikiwemo kumtimua Waziri wa Fedha Pravin Gordhan kumeleta mgogoro mkubwa haswa kutokana na na mdodoro wa kiuchumi unaoendelea nchini humo. Afrika Kusini hivi sasa imeshuhudia mahitaji muhimu yakipanda bei ikiwemo chakula, petrol, kodi na mahitaji mengineyo.
Kufuatia matatizo yote hayo yanayoendelea, mashabiki wa Arsenal kutoka Afrika Kusini wao wameamua kuua ndege wawili kwa jiwe moja baada ya kuingia mitaani na mabango ya kumpinga Zuma lakini pia na mengine ya kumtanga Arsene Wenger kuondoka.
No comments:
Post a Comment