Monday, April 10, 2017

WENGER AMTAKA CHAMBERLAIN KUBAKI ARSENAL.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger anaamini kuondoka kwa Alex Oxlade-Chamberlain kunaweza kuleta hasara kubwa na kumtaka kiungo huyo kubakia Uwanja wa Emirates. Oxlade-Chamberlain amekuwa na Arsenal toka aliposajiliwa akitokea Southampton mwaka 2011, lakini anatarajia kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu. Wenger hataki kumpoteza kiungo huyo mwneye umri wa miaka 23, ambaye amekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha wachezaji wanaotaka kuongezwa mikataba mipya akiwemo Kieran Gibbs, Mesut Ozil, Aaron Ramsey na Alexis Sanchez. Wenger amesema binafasi anadhani ni muhimu kwa Chamberlain kubakia Arsenal kwani walimleta toka mdogo na wamemtengeneza kuwa mchezaji alivyo sasa.

No comments:

Post a Comment