Monday, April 10, 2017

TIMU YACHEZESHA WACHEZAJI 12 CHINA.

LIGI daraja la pili ya soka nchini China imeingia katika utata mkubwa kufuatia timu kuchezesha wachezaji 12 uwanjani mwishoni mwa mchezo. Tukio lilitokea dakika ya 89 ya mchezo kati ya klabu ya Beijing Renhe iliyokuwa ikiongoza dhidi ya Baiding Rongda wakati mchezaji Rao Weihui bila kufahamu kuwa alitolewa alipoingia tena uwanjani na kucheza. Weihui alikuwa akipokea matibabu nje ya uwanja ambapo klabu yake ya Beijing iliamua kubadilisha na kumuingiza Han Xuan. Bila kufahamu kuwa tayari alikuwa ametolewa Weihui alirejea uwanjani baada ya kumaliza matibabu na kuendelea na mchezo hivyo kufanya timu yao kuwa na wachezaji 12 na bila waamuzi kufahamu mchezo ukaendelea kwa sekunde 40. Baada ya kupita sekunde hizo 40 ndio tatizo likagunduliwa kufuatia mashabiki wa timu pinzani kuanza kuimba kwa sauti kumuhabalisha mwamuzi kuwa kuna wachezaji 12 uwanjani. Baadae Weihui alitoka nje na mchezo kumalizika kwa Beijing kushinda bao 1-0 dhidi ya Baiding.

No comments:

Post a Comment