Monday, April 10, 2017

NYOTA WA SOKA WALIPUKA KUMPONGEZA MSHINDI WA MICHUANO YA GOFU YA MASTERS.

KUFUATIA mchezaji gofu nyota wa Hispania, Sergio Garcia kufanikiwa kutwaa taji lake kubwa la kwanza la michuano ya Masters jana, salama kutoka pembe mbalimbali duniani zimemiminika kumpongeza. Michuano hiyo mikubwa kabisa ilihitishwa jana huko Augusta kwa Garcia kufanikiwa kutwaa hilo mbele ya Justin Rose na salamu kedekede za pongezi zingine kutoka katika ulimwengu wa soka zikimiminika juu yake. Mojawapo wa nyota kadhaa waliokuwa wakifuatilia michuano na kutuma salamu zao za pongezi ni pamoja na nyota wa Real Madrid Sergio Ramos na Gareth Bale ambao walitumia mitandao yao ya kijamii kumpongeza Garcia. Mbali wengine waliotuma salamu zao ni pamoja na nyota wa kimataifa wa Uingereza na Tottenham Hotspurs Harry Kane na nguli wa zamani wa soka wa Ureno Luis Figo ambaye alituma picha akiwa pamoja na Garcia. Garcia ambaye ni shabiki mkubwa wa Madrid sasa anatakabiliwa na michuano mingine mikubwa kwa mwaka huu ile ya wazi ya Marekani itakayofanyika huko Erin Hills, Wisconsin Juni mwaka huu.

No comments:

Post a Comment