Monday, April 10, 2017

MOURINHO AMKEJELI WENGER.

MENEJA wa Manchester United, Jose Mourinho anataka kuhakikisha klabu hiyo hairidhiki na mbio za kufukuzia nafasi ya nne pekee, na kusisitiza kushinda taji la ligi ni moja ya malengo yake makubwa. United imekusanya mataji mawili msimu huu akiwa wametwaa Ngao ya Hisani mwanzoni mwa msimu na pia Kombe la EFL mapema mwaka huu. Pia kwasasa United wako hatua ya robo fainali ya michuano ya Europa League huku Mourinho akitaka mafanikio zaidi Ulaya. Akizungumza na wanahabari, Mourinho amesema pamoja na kwamba anataka kumaliza nafasi nne za juu ili waweze kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini pia wana malengo ya kushinda mataji.

No comments:

Post a Comment