Monday, April 10, 2017

MANE KUKAA NJE MIEZI MIWILI.

KLABU ya Liverpool imebainisha kuwa mshambuliaji wake Sadio Mane anatarajiwa kukaa nje kwa kipindi miezi miwili. Nyota huyo wa kimataifa wa Senegal alipata majeruhi wakati alipogongana na Leighton Baines kwenye mchezo Liverpool walioshinda mabao 3-1 dhidi ya mahasimu wao wa Merseyside Everton Aprili mosi mwaka huu. Baada ya kufanyiwa vipimo mapema leo madaktari wamedai kuwa Mane anatakuwa fiti tena baada ya kupita miezi miwili. Mane amekuwa kwenye kiwango kizuri toka tue Anfield kwa kitita cha paundi milioni 30 akitokea Southampton majira ya kiangazi mwaka jana. Nyota huyo mwneye umri wa miaka 25 amefunga mabao 13 na kusaidia mengine matano kwenye Ligi Kuu msimu huu akiwa na Liverpool.

No comments:

Post a Comment