Monday, April 10, 2017

TONY ADAMS APEWA SHAVU GRANADA.

NAHODHA wa zamani wa Arsenal, Tony Adams ameteuliwa kuwa kocha wa klabu ya Granada inayosuasua katika La Liga mpaka mwishoni mwa msimu huu. Granada ilimtimua Lucas Alcaraz kufuatia kipigo cha mabao 3-1 walichopata jana dhidi ya Valencia ambacho kimewaacha wakining’inia kwenye nafasi ya 19 katika msimamo wa ligi. Adams mwenye umri wa miaka 50 ambaye kwa kipindi chote cha soka lake amekitumia Arsenal na kushinda mataji manne ya ligi, amewahi pia kuzinoa timu za Wycombe Wanderers, Portsmouth na Gabala. Beki huyo wa zamani amecheza Arsenal kwa miaka 22 na amekuwa akihesabika kama mmoja wa wachezaji bora kabisa kuwahi kuichezea klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment