Tuesday, April 11, 2017

MUSTAKABALI WANGU HAUJAWAATHIRI WACHEZAJI - WENGER.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema utata kuhusu mustakabali wake haujaathiri wachezaji wake, lakini amekiri kipigo cha mabao 3-0 kutoka Crystal Palace kimezua wasiwasi mkubwa. Wenger anatarajiwa kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu na tayari ameshapewa ofa ya miaka mingine miwili zaidi ingawa hajatangaza kama ataendelea kuinoa timu hiyo. Arsenal kwasasa inashikilia nafasi ya sita, alama saba nyuma ya nafasi nne za juu huku kukiwa kumebaki mechi nane ligi kumalizika. Akizungumza na wanahabari, Wenger amesema amefanikiwa kuiongoza Arsenal kwenye mechi zaidi ya 1,100 na hawajazoea kupoteza namna hiyo. Wenger aliendelea kudai kuwa siku zote wamekuwa wakibadilika kwa haraka na kutokubali kushindwa. Katika mchezo huo baadhi ya mashabiki waliosafiri na timu walikuwa wamebeba mabango ya kumtaka Wenger kuondoka huku pia wakiimba kuwa wachezaji wa timu hiyo hawastahili kuvaa jezi za timu hiyo kutokana na kipigo hicho walichopata.

No comments:

Post a Comment