Tuesday, April 11, 2017

ADEBAYOR APIGA HAT-TRICK UTURUKI.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Togo, Emmanuel Adebayor amewapa pongezi wachezaji wenzake wa zamani akiwemo Cristiano Ronaldo na Thierry Henry kufuatia hat-trick aliyofunga dhidi ya Galatasaray. Adebayor alifunga mabao hayo katika ushindi wa mabao 4-0 iliyopata klabu yake ya Basaksehir ya Istanbul. Akizungumza na wanahabari, Adebayor amesema anadhani ni hat-trick yake ya kwanza toka alipokuwa Real Madrid waliposhinda mabao 8-1 dhidi ya Almeria Mei mwaka 2011. Adebayor aliendelea kudai kuwa kutokana na hilo anadhani wanastahili nguli aliocheza nao kama Dennis Bergkamp, Thierry Henry, Patrick Vierra na Ronaldo kwani alijifunza mengi kutoka kwao. Adebayor alitimkia Uturuki akiwa mchezaji huru kufuatia kushindwa kuongeza mkataba wake katika klabu ya Crystal Palace Januari mwaka huu.

No comments:

Post a Comment