Thursday, April 13, 2017

DROGBA SASA KUMILIKI TIMU MAREKANI.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Ivory Coast na Chelsea, Didier Drogba amejiunga na klabu ya Phoenix Rising ya Marekani kama mchezaji na mmiliki mwenza. Drogba mwenye umri wa miaka 39, hajacheza toka alipoondoka katika klabu ya Montreal Impact Novemba mwaka jana. Mkongwe huyo anatarajiwa kuwa kama mchezaji lakini pia kama sehemu ya wamiliki wa klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani. Akizungumza na wanahabari, Drogba amsema kumiliki timu na wakati huohuo kuwa mchezaji ni jambo lisilo la kawaida lakini analichukulia kama changamoto mpya kwake. Drogba aliendelea kudai kuwa amepata ofa nyingi kutoka China, Uingereza kwenye Ligi Kuu na ligi ya ubingwa lakini kote huko walikuwa wakimuhitaji kama mchezaji pekee.

No comments:

Post a Comment