Thursday, April 13, 2017

ALGERIA YAPATA KOCHA MPYA.

CHAMA cha Soka cha Algeria, kimemteua Lucas Alcaraz kuwa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo ikiwa ni mara ya nne kufanya hivyo katika kipindi cha miezi 13 iliyopita. Alcaraz raia wa Hispania alitimuliwa Jumatatu iliyopita kama kocha wa Granada kufuatia klabu hiyo kusuasua kwenye La Liga ikiwa mkiani kwenye msimamo. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 50 anachukua nafasi ya Georges Leekens wa Ubelgiji ambaye alijiuzulu baada ya Algeria kuenguliwa katika hatua ya makundi ya michuano ya Mataifa ya Afrika mapema mwaka huu. Mechi ya kwanza ya mashindano kwa Alcaraz itakuwa dhidi ya Togo wakati Algeria watakapoanza kampeni zao za kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2019.

No comments:

Post a Comment